Bekina nahodha wa Simba, Nassor Said ‘Chollo’,
juzi Jumamosi alishindwa kuhudhuria mazoezi ya ufukweni ya timu hiyo baada ya
kupata ajali ya pikipiki wakati akielekea mazoezini katika eneo la Ubongo
Terminal jijini Dar es Salaam.
Kikiosi cha Simba kinafanya mazoezi katika
Ufukwe wa Coco jijini Dar kwa ajili ya kusaka stamina kikijiandaa na Ligi Kuu
Bara msimu ujao inayotarajiwa kuanza Septemba 20.
Daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe, ameliambia
Championi Jumatatu kuwa, Chollo hakupata majeraha ya kutisha katika ajali hiyo.
“Nikweli
Chollo ameshindwa kufanya mazoezi ya ufuweni kwa sababu amepata ajali ya
pikipiki leo (juzi) katika eneo la Ubungo Terminal alipokuwa anakuja kwenye
mazoezi ya ufukweni, lakini hajapata majeraha ya kutisha.
“Hakuweza kuumia sana ila kubwa zaidi amepata
jeraha dogo kwenye goti pamoja na enka, hivyo nadhani Jumatatu (leo) anaweza
kuendelea kufanya mazoezi na wenzake iwapo atakuwa vizuri,” alisema Gembe.
0 COMMENTS:
Post a Comment