Pamoja na kuamua kumuacha kwa madai
alitaka fedha nyingi, sasa Simba iko katika hatua za mwisho kumnasa
mshambuliaji Mkenya, Modo Kiongera.
Habari za uhakika kutoka ndani ya
Simba, zimeeleza, Kocha Zdravko Logarusic amesisitiza kumpata mshambuliaji
huyo.
Kiongera aliwahi kufanya kazi na Loga
wakiwa Gor Mahia baada ya kocha huyo kutoka Croatia kumtwaa kwa mkopo kutoka KCB.
Simba ilianza harakati za kumnasa,
lakini ikaelezwa bei yake ilipanda baada ya mmoja wa viongozi kuwavuruga
wenzake.
Kamati ya usajili ikaamua kuachana
naye lakini msisitizo wa Loga umefanya warudi kuendelea na mazungumzo naye na
yako katika hatua za mwisho.
0 COMMENTS:
Post a Comment