Na Boniface Wambura
Kikosi cha
Taifa Stars chini ya Kocha Mart Nooij kinatarajia kuondoka keshokutwa (Julai 24 mwaka huu) kwenda Mbeya
ambapo kitapiga kambi ya wiki moja kujiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya
Msumbiji.
Mechi hiyo
ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya kushiriki Fainali za
Afrika (AFCON) zitakazochezwa mwakani nchini Morocco itafanyika wikiendi ya
Agosti 2 na 3 mwaka huu nchini Msumbiji.
Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager itaondoka nchini Julai 31 mwaka huu kwenda
Johannesburg, Afrika Kusini ambapo itafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kutua
Maputo kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimpeto.
0 COMMENTS:
Post a Comment