Mechi ya
michuano ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji (Mambas)
iliyochezwa juzi (Julai 20 mwaka huu) imeingiza sh. 158,350,000 kutokana na
washabiki 19,684 walioingia kwa kiingilio cha sh. 7,000 na sh. 30,000.
Mgawo wa
mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh.
24,155,084.75, gharama za tiketi (MaxMalipo) sh. 19,684,000, gharama za mchezo
sh. 22,902,183, uwanja sh. 11,451,092, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF) sh. 5,725,546 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh.
74,432,095.
Tunawashukuru washabiki wote waliojitokeza
kwenye Uwanja wa Taifa kuishangilia Taifa Stars katika mechi hiyo iliyomalizika
kwa sare ya mabao 2-2.
0 COMMENTS:
Post a Comment