July 24, 2014



Mashabiki wa soka wanaopinga Israel kuishambulia Palestina, jana wamevamia uwanjani wakati wa mechi ya kirafiki kati ya Lille na Macabi Haifa ya Israel na kusababisha mchezo kuvunjika.


Mwamuzi wa mchezo huo ulipigwa nchini Austria alilazimika kuumaliza katika dakika ya 86 baada ya mashabiki hao wanaoaminika wana asili ya Uturuki na palestina kuvamia na kuanza kuwatwanga wachezaji.



Hali hiyo ilisababisha ugomvi kuibuka na wachezaji hao wa Macabi Haifa nao wakaanza kujibu mapigo, hivyo ukawa ni uwanja wa ndondi.

Mwezi uliopita, Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) lilitangaza kuwa timu za Israel zisiende kucheza mechi katika nchi nyingine za Ulaya.
Lakini inaonekana agizo hilo halikutekelezwa na kusababisha tatizo hilo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic