August 19, 2014

  
Hatimaye Luis Suarez ameichezea Barcelona kwa mara ya kwanza katika mechi ya kirafiki dhidi ya FC Leon.
Barcelona ilishinda kwa mabao 6-0 kwenye Uwanja wa Cam Nou huku Lionel Messi na Neymar aliyekuwa amjeruhi wakitikisa nyavu.
Burudani kubwa ilikuwa ni Suarez aliyeingia baadaye.
Alishangiliwa kwa nguvu na mashabiki na mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool akaingia na kuonyesha mbwembwe.
Hata hivyo atalazimika kurudi benchi wakati La Liga inaanza wikiendi hii.
Atakuwa nje hadi Oktoba 26 kuitumikia adhabu yake ya Fifa kutokana na kumng’ata beki Giorgio Chiellini wa Italia wakati wa Kombe la Dunia.
‘Usamjo’ umetumika kuipoza adhabu hiyo na sasa Suarez anaruhusiwa kuendelea na mazoezi na Barcelona na pia kucheza mechi za kirafiki.















0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic