| BANDA WAKATI AKIWA COASTAL... |
Wakati Coastal Union wakiendelea kumlilia beki
Abdi Banda, mchezaji huyo ambaye amesaini mkataba wa kuichezea Simba, amepewa
nyumba ya kuishi.
Hatua hiyo imekuja siku chache tangu
mshambuliaji wa Simba, Mrundi Pierre Kwizera, kupewa nyumba ya kuishi pia
maeneo ya Kunduchi.
Banda amepewa jumba eneo la Mikocheni huku
ikikumbukwa kuwa enzi za utawala wa Mwenyekiti Ismail Aden Rage mchezaji
aliyeishi sehemu za gharama kubwa alikuwa ni straika Amissi Tambwe ambaye
alipangishiwa mitaa ya Sinza.
“Mimi si mwenyeji wa Dar, viongozi wameniambia
kuwa tayari wamenitafutia nyumba Mikocheni na ndani ya wiki hii ninaweza
kuhamia,” alisema Banda.







0 COMMENTS:
Post a Comment