Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo amesema nia
kubwa ya kwenda kuweka kambi Pemba ni kufuata vitu muhimu vitatu.
Maximo amesema
kuwa kwa siku chache alizokaa na kikosi amefurahishwa na mabadiliko ya
wachezaji wake na kusema kuwa mambo hayo matatu yakikamilika, basi kikosi chake
kitakuwa tayari kwa msimu mpya.
Kocha huyo raia wa Brazil ametaja mambo hayo
kama ifuatavyo: “Mbinu, nitaanza na suala hili kwanza kwa kuwa nitakuwa na
wachezaji wote.
“Nitatengeneza programu maalumu kwa kusaidiana
na makocha wenzangu jinsi ya kuwatumia mabeki, viungo na washambuliaji.
“Jambo la pili ni ufundi, hili nalo linatakiwa
kukamilika kabla ya mechi ya Ngao ya Hisani (dhidi ya Azam).
“Tatu ni nguvu, ili kikosi kiimarike basi
lazima wachezaji wawe na nguvu na stamina. Hayo ndiyo mambo matatu makubwa
lakini kutakuwa na vitu vingine nikiwa visiwani huko.”
Kiongozi mwingine wa Yanga aliliambia gazeti
hili kuwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ambao ni wadhamini wa klabu hiyo
wamechelewesha kuipa klabu hiyo fedha za udhamini na ndiyo maana mishahara
imechelewa pia.








0 COMMENTS:
Post a Comment