August 11, 2014

RAMA (KUSHOTO) SIKU ALIPOTUA NCHINI NA KUPOKELEWA NA MMOJA WA MABOSI WA SIMBA, MEDDY.


Bila kuchelewa, Simba imemfungashia virago mshambuliaji Jerome Ramatlhakwane maarufu kama Rama.

Mshambuliaji huyo raia wa Botswana ameondoka nchini jana kwenda kwao Botswana.
Rama alitua nchini kufanya majaribio, akapata nafasi ya kucheza katika mechi ya kirafiki kati ya Simba dhidi ya Zesco.
Simba ililala kwa mabao 3-0 katika mechi hiyo na Rama akashindwa kuonyesha uwezo.
Rama anakipiga katika kikosi cha Don Bosco ambayo imemchukua kwa mkopo kutoka TP Mazembe.


Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo, amewapiga ‘stop’ kiungo wake mshambuliaji, Andrey Coutinho na straika Genilson Santos ‘Jaja’ wote raia wa Brazil kupiga chenga na kukaa na mipira kwa muda mrefu.

Wabrazili hao walitua nchini hivi karibuni na kusaini mikataba ya miaka miwili kila mmoja kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Coutinho alisema amezuiwa kupiga chenga na kukaa na mpira kutokana na ubovu wa viwanja nchini ambavyo havikidhi mahitaji yao.
Coutinho alisema kocha wao amewataka kucheza pasi za haraka na kupiga mipira mirefu ya juu wakati wakiwa na mpira wakiwa wanashambulia lango la timu pinzani.
“Nilipofika nchini na kusaini mkataba wa kuichezea Yanga, kocha alinitahadharisha kabisa kuhusiana na ubovu wa viwanja tutakavyovitumia kuwa siyo vizuri kama vya nyumbani.
“Pia Jaja aliambiwa mapema, hivyo kutokana na hali hiyo, kocha akatuambia tusikae na mipira muda mrefu, pia tusipige chenga zisizokuwa na umuhimu, akitutaka tucheze mipira mirefu na ya juu kwa hofu ya viwanja.
“Na katika mazoezi yake, anafundisha tucheze aina hiyo ya soka akiamini kuwa ndiyo njia pekee ya kucheza sehemu yenye uwanja mbaya,” alisema Coutinho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic