August 11, 2014




 Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo, amewapiga ‘stop’ kiungo wake mshambuliaji, Andrey Coutinho na straika Genilson Santos ‘Jaja’ wote raia wa Brazil kupiga chenga na kukaa na mipira kwa muda mrefu.


Wabrazili hao walitua nchini hivi karibuni na kusaini mikataba ya miaka miwili kila mmoja kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika.

Coutinho alisema amezuiwa kupiga chenga na kukaa na mpira kutokana na ubovu wa viwanja nchini ambavyo havikidhi mahitaji yao.
Coutinho alisema kocha wao amewataka kucheza pasi za haraka na kupiga mipira mirefu ya juu wakati wakiwa na mpira wakiwa wanashambulia lango la timu pinzani.
“Nilipofika nchini na kusaini mkataba wa kuichezea Yanga, kocha alinitahadharisha kabisa kuhusiana na ubovu wa viwanja tutakavyovitumia kuwa siyo vizuri kama vya nyumbani.
“Pia Jaja aliambiwa mapema, hivyo kutokana na hali hiyo, kocha akatuambia tusikae na mipira muda mrefu, pia tusipige chenga zisizokuwa na umuhimu, akitutaka tucheze mipira mirefu na ya juu kwa hofu ya viwanja.
“Na katika mazoezi yake, anafundisha tucheze aina hiyo ya soka akiamini kuwa ndiyo njia pekee ya kucheza sehemu yenye uwanja mbaya,” alisema Coutinho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic