August 11, 2014



Mshambuliaji Hamis Kiiza tayari yuko jijini Dar es Salaam na leo ameanza rasmi kazi na kikosi cha Yanga chini ya Marcio Maximo.

Kiiza ameanza kujifua na Yanga leo kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondary ya Loyola jijini Dar, huku Mganda mwenzake, Emmanuel Okwi akiwa amesusa kuja jijini Dar.
Hadi juzi usiku, Okwi alitakiwa kuwa ametua lakini haikuwa hivyo na Kiiza akatekeleza agizo hilo.
Uongozi wa Yanga uliamua wawili hao waje nchini ili Kocha Marcio Maximo afanye kazi ya kuangalia nani ni mkali kati yao katika nafasi moja ya mchezaji wa kimataifa iliyobaki.
“Hadi jana (juzi) hakuwa amefika na hadi leo (jana), hakuna taarifa zozote,” kilieleza chanzo.
“Suala hilo limeonyesha kuudhi zaidi uongozi kwa kuwa Okwi anaonekana kuzidisha nyodo.”
Wakati chanzo hicho kinaeleza hayo, kuna taarifa Okwi amekuwa akisisitiza kulipwa fedha zake kwanza.
Lakini rafiki yake wa karibu kutoka Uganda amesema huenda pia akaja nchini ingawa amekuwa amesisitiza kulipwa fedha hizo.
Taarifa za awali zilieleza Okwi ndiye alionekana kuwa chaguo la wengi, lakini kuchelewa kwake kuja kunaifanya Yanga kugeuza uamuzi na kuangukia kwa Kiiza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic