August 22, 2014



Kocha msaidizi wa timu ya wachezaji wa zamani wa Tanzania Eleven, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, juzi  alitoa kituko kwa kumchapa kofi mwandishi ambaye (siyo wa Championi) alikuwa akimrekodi bila idhini yake baada ya kumaliza mazoezi yanayofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar.


Julio alifanya kitendo hicho baada ya kugundua anarekodiwa pasipo mwenyewe kujua, jambo ambalo lilimkera, hivyo kuchukua uamuzi huo kama alivyofanya staa wa Argentina, Diego Maradona hivi karibuni.
 
Julio alizungukwa na kundi kubwa la mashabiki ambapo alikuwa akipiga nao soga mbalimbali. Wakati mazungumzo yamekolea, kocha huyo alimpokonya simu kijana aliyekuwa karibu yake na kuitupa mbali na kisha kumpiga kibao na kumsindikizia na maneno yake yalee ya mbwembwe.

“Haiwezekani we ufike unirekodi tu mimi wakati nipo kwenye mazungumzo binafsi,” alisema Julio na kuungwa 
mkono na wale aliokuwa akizungumza nao.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic