Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio
Maximo amejikuta akitumbukia katika lindi la mawazo baada ya kuwakosa mazoezini
nyota wake, Andrey Coutinho na Kelvin Yondani.
Hali hiyo imemfanya Maximo
aonekane kuwa ni mwenye mawazo mengi kutokana na kutojua siku ambayo wachezaji
hao ambao ni kati ya nyota wake wa kutumainiwa watarudi uwanjani kuendelea na
kazi yao.
Daktari wa Yanga, Juma
Sufiani amesema wachezaji hao ni wagonjwa na ndiyo maana katika mazoezi ya jana
hawakuweza kuonekana uwanjani.
Alisema Coutinho ambaye
amejiunga na klabu hiyo hivi karibuni akitokea nchini Brazil, anasumbuliwa na
maumivu ya mgongo wakati Yondani anasumbuliwa na Malaria.
“Hata hivyo kwa sasa
wanendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu hivyo nimatuini yetu kuwa watarudi
uwanjani hivi karibuni kabla ya safari yetu ya Kisiwani Pemba,” alisema
Sufiani.
Kikosi hicho cha Yanga
kinatarajia kuonda Dar es Salaam, Jumatatu hii na kwenda Pemba kwa ajili ya
kupiga kambi ya siku 10 ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara unaotarajia
kuanza kutimua vumbi Septemba 20 mwaka huu.
SOURCE: CHAMPIONI JUMAMOSI
0 COMMENTS:
Post a Comment