August 16, 2014

MUSOTI (KULIA KWA UHURU) AKIMSIKILIZA KWA UMAKINI MKUBWA KOCHA PHIRI.


Beki wa kati wa Simba, Mkenya Donald Musoti ametamka wazi kwamba kocha wake mpya wa sasa, Mzambia Patrick Phiri yupo ‘soft’, kitu ambacho alikiri kuwa ni tofauti sana na kocha wake wa zamani wa Zdravko Logarusic raia wa Croatia.
Phiri ameanza kazi rasmi ya kuinoa Simba juzi Alhamisi, bada ya kusaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo mwaka mmoja n kuchukua mikoba ya Loga aliyefutwa kazi klabuni hapo Jumapili ya wiki iliyopita.

Musoti alifafanua kauli yake hiyo ya soft kwamba ni kocha ambaye mpole na si mkali wakati wa utendaji wake wa kazi katika kuhakikisha mchezaji anayaelewa mafuno yake kitu ambacho kimemfanya amkubali zaidi kocha huyo tofauti na Loga aliyekuwa anatumia ukali zaidi katik kuelekeza.

“Unajua huyu Phiri yupo soft sana lakini yule Loga alikuwa ‘hard’ mno katika ufundiahji wake, kila kocha ana staili yake na ujanja wake wakati wa ufundishaji, lakini nikwambie tu ukweli kamba nimefurahishwa sana na ufundishaji wa Phiri.

“Loga niliwahi kuwa nae Gor Mahia namfahamu lakini Phiri ndio kwanza nimekutana nae Simba lakini nimekuwa nikimuona na kupata taarifa zake kutoka kwenye wachezaji mbalimbali aliowahi kuwafundisha hapa Afrika Mashariki, ni kocha mzuri kwa kweli,” alisema Musoti.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic