August 11, 2014



Timu ya Mgambo JKT ya mkoani Tanga, imesema inahitaji kucheza mechi nne za kirafiki, sawa na dakika 360, kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara Septemba 20, mwaka huu.

Timu hiyo ambayo ilinusurika kushuka daraja msimu uliopita, baada ya kushika nafasi ya 11, ipo katika maandalizi ya msimu ujao ambapo imeweka kambi jeshini hapo.
Kocha wa timu hiyo, Bakari Shime, alisema timu yao inahitaji kucheza mechi nne kwa ajili ya maandalizi na kuwapima wachezaji wao wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao.
“Tupo katika maandalizi, ambapo tunatarajia kucheza mechi nyingi ili kukiandaa kikosi changu kufanya vizuri na kushika nafasi za juu katika ligi,” alisema Shime ambaye timu yake ilinusurika kushuka daraja msimu uliopita.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic