Muda wa mshambuliaji Angelo Di Maria kuondoa Real Madrid unaanza
kuhesabika.
Pamoja na kutangaza dau jipya la zaidi ya pauni milioni 70 ili
Manchester United impate, lakini inaonekana Madrid imeshindwa kumzuia.
Kwani leo asubuhi hakuonekana mazoezini na kitendo cha kocha Carlo
Ancelotti kutomjumuisha kwenye mechi za Super Cup ya Hispania, inaonyesha kiasi
gani hayuko kwenye hesabu za timu hiyo.
Siku nne zilizopita, Cristiano Ronaldo na Sergio Ramos walizungumza na
uongozi na kuutaka ufanye juhudi kumbakiza.
Lakini Muargentina huyo anaonekana kuchoshwa na kutopewa heshima yake,
hivyo anaweza kuondoka ndani ya leo au kesho.








0 COMMENTS:
Post a Comment