Mshambuliaji wa JS Kabylie, Albert Ebosse ameuwawa uwanjani wakati wa
mechi ya Ligi Kuu nchini Algeria.
Katika mechi hiyo iliyopigwa juzi, JS Kabylie iliishinda USM Alger kwa
mabao 2-1, moja likiwa limefungwa na Ebosse mwenye umri wa miaka 24.
Ilionekana mashabiki wa USm Alger ambao wamekuwa wakielezwa kuwa na
tabia za kibaguzi walirusha kitu ambacho kilimpiga kichwani akaanguka na
kupoteza fahamu, baadaye maisha.
Mechi hiyo yenye upinzani mkali ilipigwa katika eneo la Tizi Ouzou
nchini Algeria na tayari serikali ya nchi hiyo imesema imeanza uchunguzi wa
jambo hilo.








0 COMMENTS:
Post a Comment