Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeahidi kuboresha makao makuu ya
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) yaliyoko kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume,
Ilala ili yawe katika kiwango cha kisasa ikiwa ni
pamoja na kuwa na vitendea
kazi na miundombinu ikiwa ni pamoja na upanuzi
wa ofisi.
Hatua hiyo
itaiwezesha TFF kuwa na mazingira bora ya
kufanya shughuli zake kwa ufanisi.
Vilevile kupitia
programu zake mbalimbali ikiwemo ile ya Goal, Fifa imeahidi
kushirikiana na TFF
katika kuendeleza mradi wa kiuchumi kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume.
Mwanzoni mwa
mwaka huu, TFF ilihamishia makao yake makuu katikati ya
jiji ili kupisha
maendeleo ya kuiwezesha Karume kuwa kituo cha kisasa kwa
michezo na vitega
uchumi.
Akiongea
mwishoni mwa ziara ya kikazi nchini, Meneja Miradi wa Fifa
anayeshughulikia
Programu za Afrika, Zelkifli Ngoufonja amesema
Fifa inaunga mkono wazo la
kuboresha makao makuu ya Karume na itasaidia
kwa awamu uboreshaji huo.
Katika
kuhakikisha usimamizi na utekelezaji
barabara wa mradi huo, ujumbe huo wa Fifa ulikubaliana na Kamati ya
Utendaji ya TFF kuboresha ofisi za Karume ili jengo
la utawala lianze
kutumika huku mradi ukitekelezwa kwa awamu.
Pamoja na
kuongelea mradi huo muhimu kimichezo na kibiashara, ujumbe huo
uliokuwa nchini
kwa juma moja kufuatia mwaliko wa TFF ulikuwa na nafasi ya
kujadiliana na TFF
kuhusu maboresho katika masuala mbalimbali yakiwemo ya
Utawala, Fedha, Masoko,
Ufundi, Mashindano na timu za taifa.
Akiongea kwa
niaba ya Kamati ya Utendaji ya TFF, Rais wa TFF Jamal Malinzi
aliushukuru
ujumbe huo wa Fifa kwa msaada mkubwa katika historia ya
mahusiano kati ya Fifa na TFF.
Ujio huo
unafuatia maombi ya TFF kuwa sehemu ya mradi wa Performance wa
Fifa. Mradi wa
Performance unaoshirikisha nchi
mashirikisho 163 kati ya wanachama 209 wa Fifa,
unalenga kuongeza ufanisi
katika uendeshaji na uongozi wa nchi wanachama wa
Fifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment