August 18, 2014



Kutokana na presha ya usalama kuwa mdogo wakati wa mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga, Bodi ya Ligi imeamua kuongeza askari wa usalama hadi 400 kwa ajili ya kulinda amani siku watani hao watakapokutana.


Hayo yamesemwa na ofisa mtendaji wa bodi hiyo, Silas Mwakibinga, ambaye amesema kuwa wameamua kuongeza idadi ya askari hadi kufikia 400 ambao watakuwa na vitendea kazi kama farasi na mabomu ya machozi kutokana na vitendo vya fujo ambavyo vimekuwa vikijitokeza katika mechi za watani.

Simba kwa sasa ipo chini ya kocha Mzambia, Patrick Phiri huku Yanga ikiwa chini ya Mbrazil, Marcio Maximo.

 “Tanzania hatujafikia hatua ya kufungia mashabiki. Kwanza fujo za mashabiki wetu si za kuhatarisha maisha ya wachezaji kama nchi nyingine, mfano Misri, pili ‘nature’ ya mpira wetu ni wa kutegemea viingilio, hivyo tumeamua kuboresha sekta ya ulinzi msimu huu kwenye mechi kubwa,” alisema Mwakibinga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic