Kiungo mshambuliaji aliyetemwa Simba, Zahoro Pazi amesema kuwa kwa
sasa inabidi achukue uamuzi mgumu maana ndiyo itakuwa njia sahihi kwake kupata
haki yake, ambapo uamuzi huo ni kuishitaki klabu hiyo kwa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) baada ya kutopata barua au taarifa yoyote ya kumuacha kwenye
usajili.
Pazi ni mtoto wa kipa wa zamani wa Simba ambaye sasa ni kocha wa
makipa katika kikosi hicho kilichoweka kambi Zanzibar.
Pazi ni mmoja wa wachezaji waliotemwa na klabu hiyo wakiwa bado na
mikataba pamoja na wenzake Ali Badru, Edward Christopher na Betram Mwombeki na wengine ambao mikataba yao
ilikuwa imemalizika ni Ramadhan Chombo ‘Redondo’, Salum Omar, Abuu Hashimu na
Hassan Khatibu.
“Kwa sasa sina jinsi, nilichoamua ni kufuata sheria, napeleka
barua yangu kwa TFF kwa sababu Simba wameshindwa kuwa waungwana kwa kushindwa
kutimiza majukumu yao,” alisema Pazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment