Mshambuliaji Mganda, Hamisi Kiiza, ameanza rasmi
mazoezi na klabu yake chini ya kocha mkuu wa timu hiyo, Mbrazil, Marcio Maximo
ambaye anaangalia uwezo wa mchezaji huyo pamoja na wale wengine ambao wote walikuwa
wakizitumikia timu zao za taifa.
Wachezaji ambao walikuwa timu za taifa za nje ni pamoja na
Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima na Hamis Kiiza na wale wa Tanzania Kelvin Yondani, Mrisho Ngassa,
Simon Msuva, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Oscar Joshua.
Straika huyo ameanza mazoezi rasmi klabuni hapo
siku ya Jumatatu akitokea nchini kwao Uganda na kocha wa timu hiyo anataka kupima uwezo wa mchezaji huyo na kama
ataridhishwa, ataendelea naye.
Uongozi wa Yanga umemtaka kocha Maximo kuangalia
uwezo wa Waganda hao wawili kati ya Kiiza na Okwi ili wajue nani wa kumuacha
kwa jinsi alivyowaona kwa kuwa idadi ya wachezaji wa kigeni imezidi na kufikia
6 hadi sasa huku ikiwa imebaki nafasi moja pekee ya mchezaji mmoja wa nje
kuendelea kuitumikia klabu hiyo ambapo ni lazima mmoja tu afungashiwe virago.
Aidha, straika huyo alikuwa akifanya mazoezi kwa
bidii huku mara kadhaa akionekana kuwa makini na alichokuwa akielekezwa na
kocha ikiwa ni pamoja na kuzungumza naye mambo kadhaa katika mazoezi hayo.
0 COMMENTS:
Post a Comment