Kocha mkuu wa timu ya Yanga
Marcio Maximo ameweka msisitizo katika safu yake ya ulinzi baada ya kuwapa
mazoezi maalum ya uokoaji wa mipira.
Maximo anaongoza mazoezi ya
timu ya Yanga yanayo fanyika katika uwanja wa shule ya Loyola jijini Dar es Salaam.
Katika mazoezi hayo, kocha
huyo alitoa zoezi maalum kwa mabeki la kuondoa mipira ya krosi itakayopigwa na
wachezaji wa timu pinzani. Maximo alitaka kuhakikisha kila krosi itakayopigwa
katika lango la Yanga, basi mabeki wa Yanga ndio wawe wa kwanza kuicheza.
Kwa zaidi ya dakika 25,
Maximo alikua akiurusha mpira kuelekea golini huku akiwataka mabeki hao
kuuondoa katika eneo la hatari kwa kuupiga kichwa. Zoezi hilo lilikomaliwa hadi
alipoona kuwa mabeki wote wamelifanya kwa ufasaha na kwa jinsi atakavyo yeye.
Zoezi hilo liliwahusisha
mabeki wa Yanga akiwemo nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Abdul, Oscar
Joshua, Said Juma, Rajab Zahir na Issa Ngao.
0 COMMENTS:
Post a Comment