August 16, 2014




Beki wa zamani wa Yanga, Abubakari Mtiro amefanikiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Kagera Sugar ili kujiunga na jahazi hilo kukipiga katika Ligi Kuu Bara msimu ujao unaotarajiwa kuanza septemba 20, mwaka huu.


Beki huyo aliyekuwa akiitumikia klabu ya Ashanti United ameasaini katika klabu hiyo ya mkoani Kagera ambapo atakutana na beki wa zamani wa yanga Ibrahim Job kujenga ukuta imara wa klabu hiyo.
Beki huyo mwenye mwili uliojengeka kimazoezi alisema kuwa kwa sasa anamshukuru Mungu kwani timu hiyo ina mipango mizuri ambapo mpaka sasa wanaendelea vema na mazoezi kwa ajili ya kujiwinda na msimu ujao dhidi ya wapinzani wao.

“Nimesaini mkataba wa mwaka mmoja ambapo nitaitumikia klabu hii kwa kutimiza wajibu wangu ili kuleta maendeleo yenye sura mpya kwa kushirikiana na wenzangu katika suala zima la soka.

“Kwa msimu ujao Ligi Kuu Bara ninaamini ushindi tutaupata kwa juhudi mbalimbali ambazo zinaendelea katika klabu yetu huku tukijiandaa kucheza michezo kadhaa ya kirafiki kabla ya Ligi kuanza kutimua vumbi,” alisema Mtiro.   

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic