August 5, 2014


MUSONYE


Dakika tano zilizopita Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama Vya Soka Afrika Mashariki na Kati, Nicholas Musonye ametoa ufafanuzi kuhusiana na suala la Yanga na kusema anasubiri barua ya TFF.
Musonye amezungumza na Salehjembe na kusema yafuatayo:
“Siwezi kutangaza kuwafukuza Yanga kabla ya kupata barua kutoka TFF, wameniambia wataituma saa 4 hadi 5 asubuhi.
“Hivyo nasubiri na kama TFF watasema Yanga wamekubali kutuma kikosi cha kwanza, basi wataendelea na nafasi yao.
“Lakini wakisema hawawezi, basi mara moja nitatangaza kuwaondoa.
“Hii si michuano ya kudharau, naona Yanga wanafanya mchezo na kuendekeza dharau. Nafasi ya Yanga kuthibitisha ilikuwa jana usiku.
“Lakini wangefanya hivyo kupitia TFF na wao TFF watatuma barua kwetu. Kawaida tunafanya mambo kwa mpangilio na utaratibu maalum.
“Hivyo nikipata barua ya TFF, nitatoa uamuzi.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic