August 19, 2014



Ndanda inayodhaminiwa na kampuni ya Bin Slum Tyres Ltd inayotengeneza bidhaa mbalimbali za matairi kama Double Star, Vee Rubber na rim za Topu, imejigamba kuwa itafanya maajabu kwenye msimu ujao.

Kocha Msaidizi wa Ndanda, Ngawina Ngawina amesema wanaendelea kujifua vilivyo wakiwa wanajiamini kuwa watafanya vema.

“Tunalenga kufanya vizuri, tunajua ushindani mkubwa katika ligi. Lakini tutapambana na kuwashanga wengi.
“Wengi wanaweza wakatudharau lakini watashangaa,” alisema Ngawina akionyesha kujiamini.
Ndanda baada ya kupata udhamini wa Bin Slum, ni dalili kuwa italeta ushindani mkubwa.

Kikosi cha Ndanda kinaendelea kujifua kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam.
Ligi Kuu Bara imepangwa kuanza Septemba 20 na Ndanda ni kati ya timu tatu zilizopanda. Nyingine ni Stand United ya Shinyanga na Polisi Moro.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic