Na Maulid Kitenge, Msumbuji
Kocha
wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema moja ya sababu za kikosi chake kupoteza
mechi dhidi ya Msumbiji (Mambas) ni wachezaji wake kucheza kwa wasiwasi katika
kipindi cha kwanza.
Taifa
Stars iliruhusu bao la kwanza sekunde chache kabla ya kumalizika kipindi cha
kwanza katika mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika
kutafuta tiketi ya kucheza hatua ya makundi iliyochezwa leo (Agosti 3 mwaka
huu) kwenye Uwanja wa Taifa wa Zimpeto hapa Maputo.
Bao
hilo katika mechi hiyo iliyomalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao
2-1, hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-3 lilifungwa kwa kichwa na
mshambuliaji Josemar Machaisse.
Nooij
alisema wasiwasi katika kipindi cha kwanza ndio ulioipa Msumbiji fursa ya
kutawala mechi hiyo katika kipindi hicho na kukimalizia ikiwa mbele kwa bao
hilo la mshambuliaji huyo wa klabu ya Bravos de Maquis ya Angola.
Alisema
timu yake ilitulia kipindi cha pili baada ya kumuingiza Amri Kiemba badala ya
Khamis Mcha. Pia alilalamikia bao ambalo Taifa Stars ilifunga dakika ya 16
kupitia kwa John Bocco lakini likakataliwa na mwamuzi Dennis Bate kutoka
Uganda.
Aliongeza
kuwa mchezaji Elias Pelembe aliyeifungia Msumbiji bao la pili dakika ya 83 kwa
mpira wa adhabu nje ya eneo la hatari ndiye aliyemaliza mchezo huo. Pia ni
mchezaji huyo aliyebadili matokeo ya mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam
ambapo Msumbiji ilisawazisha dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na ambayo ilicheza vizuri
kipindi cha pili ilipata bao lake dakika ya 78 na Mbwana Samata kwa shuti la
pembeni akiwa nje ya eneo la hatari na kumshinda kipa Ricardo Campos.
Matokeo
hayo yameipeleka Msumbiji katika kundi C lenye timu za Cape Verde, Niger na
Zambia. Mechi za hatua ya makundi kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Afrika
zitakazofanyika mwakani nchini Morocco zitaanza kuchezwa mwezi ujao.
Mechi
hiyo ndiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya Tanzania na Msumbiji itakayoingia
hatua ya makundi ya michuano ya Afrika kwa ajili ya kutafuta tiketi za Fainali
itakayofanyika mwakani nchini Morocco.
Katika
mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita timu
hizo zilitoka sare ya mabao 2-2. Timu itakayosonga mbele itaingia kwenye kundi
lenye timu za Cape Verde, Niger na Zambia.
Taifa
Stars inarejea Dar es Salaam kesho (Agosti 4 mwaka huu) saa 8 mchana kwa ndege
ya Air Tanzania.
Kikosi cha Stars kilipangwa
hivi; Deogratias Munishi, Said Moradi, Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Nadir
Haroub, Erasto Nyoni, Mwinyi Kazimoto, Mcha Khamis/Amri Kiemba, John
Bocco/Simon Msuva, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu/Mrisho Ngasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment