Mshambuliaji Emmanuel Okwi, raia wa Uganda ambaye juzi jioni
alijiunga na Simba kudai kuwa atapambana na Wanajangwani hao kuhakikisha haki
yake inapatikana.
Maneno hayo ya Okwi yamekuja baada ya kudai
kuwa Yanga imevunja naye mkataba kisha kumfungulia mashtaka katika Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) kwa madai ya kushindwa kuzingatia makubaliano yake na
klabu hiyo kwa mujibu wa mkataba wake.
Okwi amesema atahakikisha anapambana Yanga hadi hatua ya mwisho kuhakikisha anapata haki
yake.
Alisema klabu yoyote ile inapoingia mkataba na
mchezaji inatakiwa kumlipa fedha zake zote za usajili kwa mujibu wa makubaliano
na siyo kumzungusha na kufanya mambo yake kama viongozi wake wanavyotaka.
“Sina hofu kabisa juu ya jambo hili, naamini
haki itapatikana kwa sababu hayo ambayo Yanga wananipakazia hayana ukweli
wowote na kama kuna ukweli basi kutakuwa na sababu.
“Hata hivyo kwa sasa haina haja ya kuongea
mambo mengi ila jambo la msingi ambalo ningependa kusema ni kwamba, nipo tayari
kusimama sehemu yoyote ile juu ya jambo hili ili kuhakikisha haki yangu
inapatika.
“Hata kama TFF na Fifa watanihitaji leo hii
nitasimama mbele yao na kutoa ushahidi wangu juu ya jambo hili,” alisema Okwi
ambaye Yanga imeachana naye akiwa bado na mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
Yanga ilimsajili Okwi akitokea SC Villa ya
Uganda ambayo alijiungana nayo akitokea Etoile du Sahel ya nchini Tunisia
ambayo alikuwa na matatizo nayo.
0 COMMENTS:
Post a Comment