August 30, 2014



Kiungo mkongwe Henry Joseph, amefunguka kuwa ameamua kuweka kando masuala ya soka na kujikita katika shughuli nyingine za kijamii, baada ya kusaka timu bila mafanikio.


Joseph, anayejulikana zaidi kwa jina la Shindika, aliyewahi kuichezea Kongsvinger ya Norway amekuwa akihaha kutafuta timu ya kuichezea msimu ujao tangu aachane na Simba, lakini amekosa.

Shindika amesema ambaye alikuwa pia ni kiungo wa Taifa Stars, amesema ametangaza kupotezea mambo ya soka na kuongeza kuwa ataangalia upepo tena katika usajili wa dirisha dogo.

“Kwa sasa nimeachana na kutafuta timu, nimeelekeza nguvu zangu katika shughuli za kijamii, nafikiri nitaangalia tena upepo dirisha dogo la usajili,” alisema kiungo huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic