Hatimaye makocha Patrick Phiri wa Simba na Marcio Maximo wa Yanga,
wamekutana hata kabla ya pambano la watani hao.
Wawili hao wamekutana leo kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.
Maximo kutoka Brazil alionyeshwa na Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto kuwa Phiri raia wa Zambia alikuwa jukwaani.
Naye bila ya kuchelewa, mara moja akapanda juu na kumfuata Phiri na
kupiga naye stori kwa dakika kadhaa huku wote wakionekana kuwa na furaha.
Makocha hao wawili, wamekutana kwa mara ya kwanza baada ya wote kurejea
nchini.
Kawaida wangekutana Oktoba 12 kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya
watani hao.







0 COMMENTS:
Post a Comment