Mohamed Abdallah, Zanaibar
Kikosi cha Simba kinachoongozwa na Patrick Phiri, kimeishinda Kilimani ya daraja la pili Zanzibar kwa mabo 2-1 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.
Timu hiyo inasifika kwa soka la kasi na pasi nyingi ikiwa Simba wakati
mgumu kwa muda mwingi.
Simba ndiyo ilianza kupata bao kupitia Amissi Tambwe kwa mkwaju wa
penalti lakini Kilimani wakasawazisha katika dakika ya 78.
Simba walifanikiwa kupata bao la pili katika dakika ya 84 kupitia Haruna
Chanongo.







0 COMMENTS:
Post a Comment