August 20, 2014



Real Madrid imeshindwa kuutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani baada ya sare ya mabao 1-1 dhidi ya Atletico Madrid katika mechi ya Super Cuo ya Hispania.
Kutokana na sare hiyo, maana yake timu hizo zitarudiana tena kwenye Uwanja wa Vincete Calderón.
Real walifanikiwa kupata bao katika dakika ya 81 kupitia James Rodríguez likiwa ni bao lake la kwanza akiwa na kikosi chake hicho kipya.
Lakini Atletico maarufu kama Rojiblancos walifanikiwa kusawazisha dakika saba baadaye kupitia Raúl García aliyeuzungusha mpira mitaa ya ‘far-post’.
Timu hizo mabingwa wa La Liga na wale wa Copa del Rey sasa watakutana tena Ijumaa katika mechi hiyo ya marudiano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic