August 18, 2014

PHIRI AKIWA AMEMKUMBATIA UHURU, SIKU HIYO ALIKUWA AKITAMBULISHWA KWA WACHEZAJI WA SIMBA MARA BAADA YA KUSAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA KUIFUNDISHA.


Uongozi wa Simba umemuongezea mkataba wa mwaka mmoja kiungo wake mshambuliaji, Uhuru Selemani.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya kamati ya usajili ya timu hiyo, wamemuongezea mkataba huo baada ya kocha mkuu, Patrick Phiri, kupendekeza.
Chanzo hicho kilisema, kama kiungo huyo akionyesha kiwango kikubwa msimu ujao, basi watamuongezea mkataba mwingine.

“Kocha ndiye aliyependekeza Uhuru tumbakize, hivyo tumeona tumuongezee mkataba mwingine wa mwaka mmoja ambao kama akionyesha kiwango kizuri, tutamuongezea mwingine.

“Mwanzoni tulishindwa kumpa mkataba kutokana na Logarusic (Zdravko) kumkataa akidai kuwa haridhishwi na kiwango chake,” kilisema chanzo hicho.

Uhuru ni miongoni mwa wachezaji wakongwe waliobaki katika kikosi cha Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic