NIYONZIMA (KUSHOTO) AKIWA KWENYE BENCHI LA YANGA. HII ILIKUWA NI MSIMU ULIOPITA. |
Kocha Mkuu wa Yanga, Mbrazili, Marcio Maximo,
amemuangalia kiungo wake mchezeshaji, Mrwanda, Haruna Niyonzima na kuamua
kumtoa kati na kumpeleka pembeni.
Mbrazili huyo, katika mazoezi ya hivi karibuni
yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Loyola, Mabibo jijini Dar es Salaam, alimpanga
Niyonzima kucheza namba saba huku nane akimchezesha Hassani Dilunga.
Maximo alimpanga Niyonzima kucheza nafasi hiyo
mara baada ya kupanga vikosi viwili vilivyocheza mechi, kati ya hivyo, kimoja
alionekana kuwajaza mastaa wengi kinachodaiwa ndiyo anakiandaa kwa ajili ya
kukitumia kwenye msimu ujao.
Wakati mazoezi hayo yanaendelea, kocha huyo
alionekana akimpa maelekezo Niyonzima pamoja na beki wa pembeni, Juma Abdul
aliyekuwa anacheza namba mbili.
Pia, alionekana kumpa maelekezo kadhaa Dilunga
akimtaka kucheza kwenye eneo lake la kati muda wote huku Mbuyu Twite akimsaidia
kwenye dimba la kati (namba sita).
Alipoulizwa kocha huyo kuhusiana na sababu za
kumbadilisha namba Niyonzima kutoka namba nane hadi saba, alisema: “Katika
kikosi changu ninataka kila mchezaji awe na uwezo wa kucheza nafasi mbili hadi
tatu na siyo moja pekee.
“Sitaki mchezaji anayeweza kucheza nafasi moja
pekee, hiyo itanisaidia siku moja ikitokea mchezaji mmoja amepewa kadi nyekundu
au majeruhi, basi mwingine anamrithi.”
0 COMMENTS:
Post a Comment