![]() |
| MGOSI WAKATI AKIWA SIMBA |
Mshambuliaji mkongwe wa Mtibwa Sugar, Mussa Hassan Mgosi na
kiungo mkabaji wa timu hiyo, Vincent Barnabas, mapema wiki hii walitoa kali
baada ya kugombea vitumbua mara baada ya mazoezi katika Uwanja wa Bora,
Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Wachezaji hao waliokuwa wamekaa pembeni mwa
uwanja huo, walianza kuvishambulia vitumbua hivyo vilivyokuwa kwenye gari aina
ya Noah huku wakivisifia kuwa vimepikwa vizuri na kumsifia mpishi wa msosi huo.
“Kiukweli vitumbua ni vitamu sana, usipoangalia
unaweza kujikuta unakula mpaka ukavimbiwa, huyu mama aliyepika kavipatia sana,”
alisikika Barnabas akimwambia Mgosi huku wachezaji wengine nao wakipaza sauti
kuomba wasimaliziwe vitumbua hivyo.
Wakati huohuo, katika mazoezi ya timu hiyo, kocha msaidizi wa timu hiyo, Zuberi
Katwila, aliwataka wachezaji kucheza kwa umakini mkubwa kwa kuwa hawajapata
daktari.
“Timu bado haijapata daktari wa kudumu,
nimewaambia wawe makini,” alisema.








0 COMMENTS:
Post a Comment