August 15, 2014



Uongozi wa Yanga umefunguka kuwa upo mbioni kusaka timu kwa ajili ya mechi ya kimataifa ya kirafiki katika nchi za Afrika Magharibi, ambapo baadhi ya nchi ni Ivory Coast na Nigeria.


Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, ameliambia gazeti hili kuwa, wapo katika harakati za kusaka timu ambayo wanaiona itakuwa na kiwango kizuri ya kuweza kujipima nayo kuelekea msimu wa 2014/15.

“Kocha anahitaji kucheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa kabla ya kuanza kwa ligi, jambo ambalo uongozi tunalifanyia kazi.

“Tutatafuta kutoka nchi za Afrika Magharibi, Kusini, Mashariki na Afrika ya Kati, lengo ni kupata timu bora zitakazotusaidia kuwapima wachezaji wetu vizuri,” alisema Njovu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic