August 19, 2014



Waamuzi wanaotarajia kuchezesha mechi za Ligi Kuu ya Bara na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu huu watafanya mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) mwezi ujao.


Mtihani huo utahusisha waamuzi wa daraja la kwanza (class one) wakiwemo pia wale wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa).

Mbali ya mtihani huo unaotarajiwa kufanyika kabla ya Septemba 10 mwaka huu, pia kutakuwa na semina kwa makamishna ambao watasimamia mechi za VPL na FDL.

Hivyo waamuzi wote wanatakiwa kutumia muda uliobaki kufanya maandalizi kwa ajili ya mtihani huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic