Mshambuliaji wa Stoke City,
Biram Diouf aliyefunga bao pekee wakati timu yake ilipoitwanga Man City kwenye
Ligi Kuu England wikiendi iliyopita, leo ameibeba timu yake ya taifa ya
Senegal.
Mechi hiyo ilikuwa ni ya hatua ya makundi kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika.
Diouf amefunga bao la
kwanza wakati Senegal ilipoitwanga Misri kwa mabao 2-0 jijini Dakar na kushika
uongozi wa kundi G kuwania kucheza kombe la Mataifa Afrika.
Mkali huyo ambaye ni mshambuliaji wa Man United, aliwazidi kasi mabeki wa Misri kabla ya kumzidi kipa ujanja na kuukwamisha mpira wavuni.
Baada ya bao lake katika
dakika ya 19, Sadio Mane naye alifunga la pili katika dakika ya 45.
Juhudi za Misri kusawazisha
katika kipindi cha pili hazikuzaa matunda na sasa wanategemea mechi nyingine
kujirekebisha.
Katika mechi nyingine,
Afrika Kusini imefanikiwa kuongoza kundi A baada ya kuichapa Sudan kwa mabao
3-0.
Wasauzi wakiwa ugenini Kharthoum wamewafunga mabao yao kupitia Villakazi aliyefunga mawili na Ndulula moja.
Wasauzi wakiwa ugenini Kharthoum wamewafunga mabao yao kupitia Villakazi aliyefunga mawili na Ndulula moja.
Nayo Guinea ikiwa nyumbani
iliifunga Togo kwa mabao 2-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment