Uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro, umemzuia
mshambuliaji wao, Juma Luizio kwenda kucheza soka la kulipwa katika klabu ya
Zesco ya nchini Msumbiji baada ya kupeleka jina lake TFF kwa ajili ya kumtumia
msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
SALEHJEMBE iliona jina la Luizio ambaye alifuzu kuichezea
Zesco hivi karibuni na kusaini mkataba wa miaka mitatu, likiwa sehemu ya majina
ya usajili yaliyowasilishwa na kikosi hicho cha Manungu kuwa ni mmoja kati ya
nyota watakaoitumikia timu hiyo msimu ujao.
Mkratibu wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser, alisema uhamisho
wa mchezaji huyo bado haujakamilika ndiyo maana wamepeleka jina lake TFF kwa
madai kuwa bado ni mchezaji wao halali na watamtumia msimu ujao unaotarajiwa
kuanza kutimua vumbi Septemba 20 mwaka huu.
“Luizio bado ni mchezaji wetu halali kwa sababu usajili
wake wa kwenda Zesco haujakamilika
ndiyo maana tumepeleka jina lake TFF ili kumtumia kwenye
ligi kuu.
“Timu ya Zesco United walipocheza na timu ya Simba
ilikuwa ni mechi ya kirafiki ndiyo maana na yeye alicheza mchezo ule siyo mechi
ya ligi,” alisema Bayser.
Hivi karibuni mchezaji huyo aliliambia gazeti hili kuwa
amemalizana kila kitu na Zesco ambapo alidai kuwa amesaini mkataba wa miaka
mitatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment