Kiungo mshambuliaji
Emmanuel OKwi aliyeingia mkataba wa miezi sita na Simba, amekuwa kivutio kwenye
mazoezi ya kikosi hicho.
Katika mazoezi ya Simba
yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uninio, Bunju jijini Dar, Okwi alikuwa kivutio
kutokana na kasi na chenga zake za maudhi.
Mashabiki wengi
waliojitokeza walionyesha kuvutiwa naye na wakati mwingine walimpigia makofi
kuonyesha kukubali alichokuwa akifanya.
Okwi anatarajia kuwa katika
kikosi cha Simba kitakachoivaa Gor Mahia kwenye Uwanja wa taifa katika mechi ya
kirafiki leo jijini Dar.
0 COMMENTS:
Post a Comment