September 7, 2014


Nahodha mpya wa Brazil, Neymar Jr ameonyesha uungwana wa kimichezo baada ya kukubali kumsamehe beki Juan Zuniga wa Colombia.

Zuniga ndiye aliyemuumiza kwa kumvunja Neymar Jr mfupa mdogo wa mgongo na kumfanya aondolewe kwenye michuano ya Kombe la Dunia hatua ya robo fainali.

Lakini katika mechi ya kirafiki ya timu hizo juzi mjini Miami, Marekani ambayo Brazil ilishinda bao 1-0, Neymar alizungumza vizuri na Zuniga na baadaye kumkumbatia.
Hali hiyo ilionyesha kiasi gani ameamua kumsamehe na alimsalimia tena baada ya mchezo.

Mechi hiyo ilikuwa ni ya kwanza kwa Neymar kupewa unahodha na Kocha Mpya, Dunga. Colombia nao wakampa Zuniga unahodha wa mechi hiyo.

Wanamichezo wengi wamemsifia Neymar Jr kwa kuonyesha ukomavu huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic