Rais wa Shirikisho la Soka
Ulaya (UEFA), Michel Platini amesema Bayern Munich italazimika kutoa adhabu ya
kumsimamisha Franck Ribery kucheza mechi tatu iwapo atagoma kuichezea Ufaransa.
Riberry ametangaza kustaafu
kuichezea Ufaransa akisisitiza ni wakati wa kuwaachia vijana.
Lakini Platini ambaye ni
nyota wa zamani wa Ufaransa amesema mwenye chaguo la kucheza au la ni kocha,
kwamba amtumie yupi lakini mchezaji hawezi kukataa kuichezea timu ya taifa kama
ameitwa.
Kocha wa Les Bleus (Ufaransa),
Didier Deschamps amemchagua Ribery kwenye kikosi chake.
'[Kwa Ribery] hana uwezo wa
kuamua kujiunga au kutojiunga na timu ya taifa kama kocha wake Didier Deschamps
amemuita.
'Hii iko wazi kwenye kanuni
za Fifa, kama akikataa basi Bayern Munich wanatakiwa kuchukua hatua. Mimi hata
simuelewi, Michuano ya Ulaya itafanyika Ufaransa mwaka 20I6,” alisisitiza
Platini.
Kauli hiyo ya Platini
imeonyesha kuwashitua wengi na hasa kuhusiana na suala la kumlazimisha mchezaji
kujiunga na timu ya taifa wakati alijiuzulu kwa hiari yake.
Ribery alikosa michuano ya
Kombe la Dunia nchini Brazil wakati Ufaransa ilipotolewa kwenye hatua ya robo
fainali ya Kombe la Dunia nchini Brazil kutokana na kuwa majeruhi.







0 COMMENTS:
Post a Comment