Kipa Hussein Sharrif maarufu kama Casillas sasa
ndiye atadaka katika mechi ya watani wao Yanga itakayopigwa Oktoba 12.
Hiyo inatokana na kuvunjika kidole kwa kipa
namba moja wa Simba, Ivo Mapunda, leo mazoezini.
Daktari wa Simba, Yassin Gembe amethibitisha
kuwa Ivo amevunjika kidole na atatakiwa kukaa nje kwa wiki nne.
Kutokana na kuvunjika kwa Ivo, Simba imeanza
kumuandaa Casillas kisaikolojia kwamba yeye ndiye anapaswa kuchukua mikoaba ya
Ivo kuanzia mechi ya Jumamosi dhidi ya Polisi Moro.
“Kweli tumeanza kuzungumza na Casillas na
kumueleza kuhusiana na majukumu muhimu yaliyo mbele yake.
“Yeye ndiye anakuwa namba moja na atanakiwa
kuwa makini na kutekeleza majukumu yake.
“Kuumia kwa Ivo ni ajali kazini, lakini bado
tunaamini yeye ana uwezo mkubwa wa kuisaidia timu kuanzia mechi ya Jumamosi,
ile ya Stand, Yanga na kuendelea.
“Kikubwa Simba inataka kushinda sasa baada
ya kuanza kwa sare, tunajua tunajitaji pointi tatu muhimu,” kilieleza chanzo
kutoka ndani ya Simba.
Simba imekuwa ikiandamwa na majeruhi
mfululizo baada ya kuumia kwa Paul Kiongera, Haruna Chanongo na Issa Rashid ‘Baba
Ubaya.
0 COMMENTS:
Post a Comment