BIN KLEB (KUSHOTO) AKIWA NA NIYONZIMA. |
Mmoja wa wanachama
maarufu wa Yanga, Abdallah Bin Kleb amefunguka kuhusiana na suala lake la
kutokuwa kwenye kamati za Yanga hadi aliporejeshwa siku chache zilizopita.
“Nilimuomba Yusuf
(Manji) asiniweke kwenye kamati yoyote kwa kuwa nilikuwa nimebanwa na majukumu
yamenibana.
“Lakini baadaye
niliombwa kurejea tena kwa lengo la kushirikiana,” alisema akifafanua.
Awali kulikuwa na
taarifa kwamba Bin Kleb aliachwa kwenye kamati za Yanga kutokana na kutoelewana
na Manji.
Hata hivyo
ilifafanuliwa na viongozi wa Yanga kuhusiana na ombi lake la kuomba aachwe nje
ya kamati hizo kutokana na kubanwa na majukumu.
Lakini sasa Bin Kleb
amefunguka mwenyewe na kuweka mambo hadharani akimaliza ubishi.
0 COMMENTS:
Post a Comment