Thika United imetua
jijini Dar tayari kwa mechi yake ya kesho dhidi ya Yanga ambayo itakuwa ni ya
kwanza ya kirafiki ya kimataifa ya Marcio Maximo.
Mbali na hivyo, mechi
hiyo itakuwa ni ya kwanza ya Maximo akiwa na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa.
Pia itakuwa ya kwanza
ya Maximo katika ardhi ya Tanzania Bara baada ya kuingoza Yanga katika mechi za
kirafiki, zote zikiwa zimepigwa visiwani Zanzibar.
Thika kutoka Kenya
itakipiga na Yanga katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar.
George Otieno ambaye
ni mmoja wa maofisa wa Thika amesema lengo lao ni kuta kuifunga tu Yanga.
“Sisi tuko vizuri na
tunachotaka ni ushindi, hatuwezi kufunga safari kutoka Kenya kuja kushindwa.
“Tunajua Yanga ni
timu kongwe kuliko sisi, bora kwa maana ya ukongwe lakini kiwango chetu kipo
juu zaidi,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment