Kikosi cha Mbeya City
inayodhaminiwa Kampuni ya Bin Slum Tyre kinaonekana kupania kufanya vizuri
zaidi msimu ujao baada ya kuweka kambi nje ya mji.
“Tumeamua kuweka
kambi nje ya mji wa Mbeya kwa ajili ya kujiimarisha zaidi na mwalimu Juma
Mwambusi anaendelea na maandalizi.
“Lengo ni kucheza
michuano ya kimataifa ukizingatia Mbeya City ni kati ya timu zinazotupiwa macho
na wengi.
“Hivyo lazima
kujiandaa vilivyo na tunataka kufanya vizuri ingawa tunajua si kazi lahisi,”
alisema Dismas.
Mbeya City ilimaliza
msimu uliopita ikiwa katika nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa Azam FC na Yanga
walioshika nafasi ya pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment