CHUJI AKIWASILI KWENYE UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE LEO MCHANA HUKU SALEHJEMBE IKIENDELEA KUPATA PICHA ZA KI-INTELEJENSIA. |
Ilikuwa ubishi huku baadhi
ya vyombo vya habari vikipinga, lakini SALEHJEMBE ilishikilia msimamo wake kuwa
Athumani Iddi ‘Chuji’ anakwenda kucheza soka Oman.
Pamoja na wengi kupinga,
hilo limethibitika leo baada ya Chuji kuondoka leo mchana na ndege ya Oman Air.
Chuji anakwenda kukipiga
katika klabu kongwe ya Oman Club ambayo imeporomoka daraja hadi la kwanza.
Oman Club inataka kucheza
Ligi Kuu Oman tena kwa kuwa ndiyo moja ya klabu kongwe wapinzani wakubwa wa
Fanja FC.
Chuji ameiambia SALEHJEMBE
hivi: “Siku imewadia babu, nimejifua kwa muda mrefu na sasa nakwenda kufanya
kazi.
“Sitaki kusema mengi,
namuomba Mungu anijaalie nifanye kazi yangu vizuri.”
Awali kulikuwa na taarifa
kwamba Chuji anataka kusajiliwa Azam FC, lakini SALEHJEMBE likasisitiza
aliombewa kujifua ili awe fiti kabla ya safari ya Oman.
Wengine wakasisitiza
anatafuta namba Azam FC na ina mpango wa kumsajili, haikuwa hivyo na uhakika
ndiyo huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment