September 11, 2014


Uongozi wa klabu ya FC Lupopo ya DR Congo umesema Yanga imewadhulumu fedha kwa ajili ya usajili wa Twite.

Mmoja wa viongozi wa FC Lupopo amesema Yanga walitakiwa kulipa dola 15,000 kama wamemuongezea mkataba Twite.
"Lakini hawajafanya hivyo na nimekuja hapa viongozi wao Seif (Magari) na Abdallah (Bin Kleb) hawataki kulimaliza hili suala.
"Mwanzo walisema hawataki maneno na sisi lakini mkataba unaonyesha mchezaji ni wetu na anacheza kwao kwa mkopo tu.
"Kama waliona wanataka kuongeza mkataba lazima watulipe, tumewasiliana na chama chetu cha soka, ndiyo maana nimekuja hapa.
"Lakini naona wanatuzungusha, tutasonga mbele hadi Fifa," alisema akisisitiza amefika hadi TFF lakini mambo yanaonekana ni magumu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic