Mwanariadha maarufu mlemavu
wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius amefutiwa mashitaka ya mauaji ya aliyekuwa mpenzi wake, Reeva
Steenkamp.
Pistorius kupitia mlango wa
choo alimlipiga mwanamitindo huyo risasi nne ziliztoa uhai wake lakini akasema
alidhani wameingiliwa na mpenzi wake alikuwa chumbani kwao.
Lakini jaji Thokozile
Masipa aliyekuwa anaendesha kesi hiyo kwenye mahakama ya Pretoria, Afrika
Kusini amemfutia mashitaka ya mauaji kwa madai upande wa ushahidi haukutoa
vilelezo vilivyojitosheleza.
Akisoma hukumu yenye kurasa
3,000 Jaji Masipa alisema mwanariadha huyo angeweza kupatikana na hatia kama ushahidi
ungejitosheleza.
Alisema kutokana na
ushahidi wa kila upande inaonekana mwanariadha huyo hakukusudia kwa kuwa
alijaribu kujilinda.
Hata hivyo bado Pistorius
atalazimika kusubiri kipande kingine cha kesi hiyo kuhusiana na kifo hicho.
Hivyo kimsingi kuna kesi
ambayo itaendelea kusikilizwa baada ya yeye kuonekana hana hatia ya mauaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment