Na Saleh Ally
BURUDANI inazidi kupanda
juu katika Ligi Kuu England kutokana na usajili wa wachezaji kutoka karibu kila
upande.
Kila anayekwenda Premier
League lazima awe ana uhakika wa ubora wa kiwango chake, la sivyo nafasi ya
kucheza itakuwa hadithi.
Mshambuliaji Diego Costa ,25,
kutoka Atletico Madrid alipotua Chelsea alikuwa gumzo na ameonyesha kuwa
atapachika kweli mabao baada ya kufunga manne.
Sasa Costa anakuwa gumzo
zaidi baada ya Radamel Falcao kutua Manchester United, ikionekana sasa amepata
mshindani mwingine ambaye alikuwa mkali zaidi yake wakati wakikipiga pamoja
Atletico Madrid.
Ingawa rekodi za ufungaji
za Falcao msimu uliopita hazikuwa nzuri kutokana na kuandamwa na majeraha,
lakini kazi yake inajiulikana.
Walikuwa pamoja na
iljulikana Falcao ni mkali zaidi, akaondoa, Costa naye atatamba. Sasa
wamekutana tena ingawa kila mmoja ana upande wake ndani ya ligi moja.
Walikuwa wote:
Costa ndiye aliyefuata
nyayo za Falcao mara tu alipoondoka Atletico Madrid na kujiunga na AS Monaco
akiwa ameingoza timu hiyo kufanya vizuri hadi kutwaa Kombe la Europa.
Lakini wakati Falcao alipojiunga
na Atletico Madrid wakati wa majira ya joto mwaka 2011, Costa ndiyo alikuwa
anaondoka kwenye klabu hiyo.
Costa alikuwa amekubaliana na
Besiktas ya Uturuki kujiunga nayo, lakini baadaye akaumia goti la mguu wa kulia
na kulazimika kukaa nje kwa miezi sita, safari ya Uturuki ikaahirishwa.
Aliendelea kujiuguza na
aliporejea dimbani, alimkuta tayari Falcao akiwa ameshika ‘ufalme’ wa kupachika
mabao, hali iliyosababisha Costa apelekwe kwa mkopo katika kikosi cha Rayo
Vallecano kilichokuwa kinapambana kuokoka kuteremka daraja.
Costa akataka kuonyesha
kweli yuko safi kwa kusunga mabao 10 katika mechi za mzunguko wa pili na mwisho
akaiokoa Rayo kuteremka daraja.
Atletico wakaamua
kumrudisha kumsaidia ‘Field Marshall’ Falcao. Akiwa kwenye benchi katika mechi
ya kwanza tu, Costa alimshuhudia Falcao akitupia bao tatu ‘hat-trick’ katika
mechi ya Super Cup ya Uefa waliyoshinda kwa mabao 4-1 dhidi ya Chelsea
waliokuwa mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lakini hii ilikuwa kengere kwa viongozi wa Atletico kwamba Falcao
alikuwa anaondoka kwenda kujiunga na Monaco.
Kikubwa walichofanya ni
kujiamini na kuwashangaza wengi kwamba Costa ana nafasi ya kufanya vizuri na
kuanzia hapo alipewa nafasi ya kushirikiana kwa ukaribu kabisa na Falcao
uwanjani.
Hata alipoondoka Falcao,
kweli Costa alikamata usukani na kufanya vizuri sana. Hawakuingia fainali ya
Copa del Rey lakini walibeba ubingwa wa La Liga na kufika kwenye fainali ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Hii ilionyesha kiasi gani
Costa pia ni kifaa na kuzua mjadala kwamba wawili hao nani alikuwa mkali zaidi.
Wakati walifanya kazi kama
kiongozi na msaidizi wake, sasa wana kazi ya kuonyesha ubora nani ni zaidi kwa
kuwa kila mmoja ni kiongozi wa mashambulizi wa timu kubwa ya England.
Kwa kuwa wanakutana Costa
akiwa Chelsea na Falcao akiwa na Man United, kutakuwa na kazi lahidi ya
kuthibitisha hilo kwa kila mmoja kutokana na mabao atakayofunga.
Costa ambaye ameishacheza
mechi tatu akiwa na Chelsea tayari amepachika mabao manne mguuni. Falcao
hajacheza hata moja na atakuwa na kibarua kigumu cha kuiinua Man United, lakini
kuthibitisha kweli yeye ni Field Mashall kweli na Costa ni ‘kijana’ wake tu.
Wakiwa Atletico hakukuwa na
Di Maria, Mata au Rooney kwa Falcao, pia hakukuwa na a Cesc Fabregas, Eden
Hazard au Oscar. Hao ndiyo watakaocheza nao sasa na kila mmoja atajiongeza na
kipaji chake kuthibitisha kweli anaweza.
Oktoba 26:
Kama wote watakuwa fiti,
yaani si majeruhi, Oktoba 26 kwa mara ya kwanza wawili hao watakutana Old
Trafford wakati timu hizo zinakutana kwa mara ya kwanza msimu huu.
Kila mmoja ataonyesha
anavyoweza kuichambua difensi ya mpinzani wake na kufunga ili kuthibitisha ni
bora ya mwenzake. Yote hii ndiyo raha ya Premier League.
TAKWIMU ZA MECHI&MABAO:
Msimu wa 2013-14
Falcao:
Mechi Mabao
22
13
Costa:
Mechi Mabao
52
36
0 COMMENTS:
Post a Comment