RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI. |
Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana hivi
karibuni imekubali mapendekezo ya Kamati ya Mashindano ya kurejesha michuano ya
Ligi Daraja la Pili (SDL).
Lengo
la kurejesha ligi hiyo ni kuongeza wigo wa mashindano kitaifa ambapo itasaidia
kushirikisha kundi kubwa zaidi la wachezaji kwenye mashindano makini
yanayozingatia viwango na vigezo ili kuwapa wachezaji maendeleo ya kiuchezaji
ikiwemo kuendelezwa vipaji vyao kitaalamu.
Ligi
hiyo yenye timu 24 itachezwa katika hatua ya makundi manne ya timu sita sita
kwa mtindo wa nyumbani na ugenini ambapo mshindi wa kila kundi atapanda kucheza
Ligi Daraja la Kwanza (FDL). Timu ya mwisho kila kundi itarudi kwenye ligi ya
mkoa wake.
Hatua
ya pili ni kutafuta bingwa wa SDL ambapo timu zilizoongoza makundi (nne)
zitacheza kwa mtoano nyumbani na ugenini. Utakuwepo mchezo wa fainali ambapo
mshindi atkuwa bingwa wa SDL msimu wa 2014/2015.
Timu
zitakazocheza SDL kwa msimu huu ni zile zilizoshika nafasi ya pili hadi ya nane
katika Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) katika makundi yao msimu uliopita, na
tatu zilizoshuka kutoka FDL msimu uliopita.
Kundi
A litakuwa na timu za Milambo FC (Tabora), Mji Mkuu FC (Dodoma), Mpanda United
(Mpanda), Mvuvumwa FC (Kigoma), Singida United (Singida) na Ujenzi (Rukwa).
Kundi B ni Arusha FC (Arusha), Bulyanhulu FC (Shinyanga), Eleven Stars
(Kagera), Mbao FC (Mwanza), Pamba FC (Mwanza) na Rwamukoma JKT (Mara).
Timu
za kundi C ni Abajalo (Dar es Salaam), Kiluvya United (Pwani), Kariakoo FC
(Lindi), Mshikamano FC (Dar es Salaam), Navy FC (Dar es Salaam) na Transit Camp
(Dar es Salaam). Kundi D ni Magereza FC (Iringa), Mkamba Rangers (Morogoro),
Njombe Mji (Njombe), Town Small Boys (Ruvuma), Volcano FC (Morogoro) na Wenda
FC (Mbeya).
Ligi
itachezwa kuanzia Novemba mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment